Jumamosi 12 Aprili 2025 - 17:45
Kugusa maandishi ya Qur'ani mtoto mdogo

Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu amejibu swali la kifiqhi kuhusu "mtoto mdogo kugusa Qur'ani.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, hadhrat Ayatollah Ali Khamenei ametoa jibu la swali lililohusu “hukumu ya mtoto kugusa Qur'ani,” jawabu lake nalo ni kama ifuatavyo.

Kugusa Qur'ani Mtoto mdogo

Swali:
Ikiwa mtoto atafungua Qur'ani na kugusa aya kwa mkono wake, sisi tunapaswa kufanya nini? Je, ni lazima tumchukue Qur'ani japokuwa kufanya hivyo kutamfanya alie?

Jawabu:
Kugusa maandiko ya Qur'ani si haramu kwa mtoto, na si wajibu kwa waliobaleghe kumzuia mtoto asiguse maandiko ya Qur'ani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha